Wakutana kuweka mikakati mabadiliko tabianchi

WADAU wa mtandao wa mabadiliko ya tabianchi na jinsia wamekutana kujadili namna bora ya kufanya kazi kwa pamoja, ili kukabiliana na madhara yanayoletwa  na mabadiliko ya tabianchi.

 

Wakichangia katika mjadala huo jijini Dar es Salaam, baadhi ya  wadau wa mtandao huo wamesema tatizo la mabadiliko ya tabianchi ni mtambuka, ambalo linahitaji bajeti kubwa ya rasilimali fedha zitakazoweza kusaidia kuongeza hamasa katika kukabilaina na changamoto hizo ndani ya jamii.

“ Ule utayari wa kushirikiana na asasi za kiraia tunaona tukija pamoja na tukawa na sauti ya pamoja na tukimuweka mwanamke mwenyewe,vijana na makundi mengine tukaweza kuwa sehemu ya changamoto na makundi tunayoyafikia kwa kushirikiana na wadau wengine  tunaweza kufikia malengo ambayo yataweza kufanya rasilimalifedha sio tu nadharia, lakini uhalisia,”anasema Mkurugenzi wa Wated, Maria Matui.

Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya CCM Mkoa wa Dodoma, Fatma Hassan  Taufic  anasema serikali imeendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo kushirikiana kutafuta rasilimali fedha ili kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi lakini bado hakuna taarifa sahihi za matumizi ya fedha hizo.

“ Kumbe bado hakuna taarifa za kutosha kuhusiana na masuala ya financing kuhusiana na masuala ya  climate change  kuna pesa ambazo zinatolewa katika category tofauti tofauti sasa hizi lazima zijulikane?  Anahoji Taufic

Naye Ofisa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira, Evansia Shirima amewahamasisha wadau hao kuongeza jitihada katika kuandika mapendekezo ya miradi mbalimbali ya kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi, ili kuongeza jitihada za utafutaji wa rasilimali fedha zitakazoweza kusaidia kuongeza uhamasishaji wa kudhibiti changamoto za mabadiliko ya tabianchi.

“ Tunaendelea kutoa elimu na kuendelea kuandaa warsha mbalimbali na wadau wa mazingira zikiwemo asasi za kiraia sekta binafsi pamoja na taasisi binafsi ambazo zinahusiana na masuala  ya jinsia na mabadiliko ya tabianchi nia kubwa na lengo kubwa kuwapa uelewa kuhusu namna gani watkavyoaanda  maandiko yao ya kuweza kupata  fedha katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi,” alisisitiza afisa huyo wa mazingira.

Habari Zifananazo

Back to top button