‘Wakuu wa Mikoa saidieni utoaji haki’

JAJI Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, amewataka wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya nchini kujua muundo na utendaji wa mahakama nchini, ili kusaidia kukabili changamoto zinazojitokeza katika mchakato mzima wa kusimamia na kutoa haki wa mahakama.

Jaji Mkuu amesema hayo mkoani Kigoma, akifungua mkutano wa Tume ya Utumishi ya mahakama na Kamati za Maadili za Mahakama za Mkoa Kigoma na wilaya zake na kubainisha kuwa, viongozi hao wana nafasi kubwa katika kushughulikia changamoto zinazojitokeza katika utoaji haki.

Profesa Juma amesema kuwa ukosefu wa mahakama katika baadhi ya wilaya nchini unachangia kuchelewesha utoaji haki katika mahakama nchini, hivyo wakuu wa mikoa na wilaya wanayo nafasi kubwa ya kuzungumzia jambo hilo kwa mamlaka mbalimbali, serikali na wadau wa maendeleo sambamba na kusimamia utekelezaji wake.

Pia Jaji Mkuu alitolea  mfano wa ukosefu wa mkongo wa Taifa katika baadhi ya wilaya, ambao umesababisha utekelezaji wa mpango wa uendeshaji wa mashauri  kwa njia ya video almaarufu  mahakama mtandao kukwama na hivyo kuchelewesha utoaji haki.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button