Walimu 54,000 kupandishwa madaraja

MBINGA – WALIMU 54,000 nchini walioachwa nyuma kimadaraja, wanatarajia kupandishwa madaraja ifikapo Julai 2024 kuleta usawa wa madaraja kwa kuzingatia kiwango cha elimu na muda wa ajira. K

auli hiyo imetolewa jana na Ofisa Elimu Mkoa wa Dodoma, Vicent Kayombo aliyemwakilisha Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serilali za Mitaa (TAMISEMI) wakati akizungumza na walimu wakuu, wakuu wa shule na maofisa elimu kata wa Mkoa wa Ruvuma.

SOMA: Wananchi wampongeza Samia kuanza safari SGR

“Katibu Mkuu Tamisemi amenituma niwaambie kwanza serikali inatujali sisi walimu haijatusahau inataka walimu wote wawe kwenye hali sawa ikilinganishwa na kiwango cha elimu na madaraja yao,” alisema.

Aliwataka walimu hao kutimiza majukumu yao ya kusimamia malezi ya wanafunzi kuhakikisha wote wanapata umahiri badala ya kuwakatisha tamaa.

“Kuna baadhi ya walimu wenzetu hawatimizi majukumu yao wengine wanadiriki hata kuwaambia wanafunzi hili somo la sayansi ni gumu hakuna somo gumu tuache huo ushamba fikiria angekuwa mwanao ungefanyaje,” alisisitiza.

Habari Zifananazo

Back to top button