Waliofia Kariakoo kuangwa mchana huu

DAR ES SALAAM – Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuongoza waombolezaji katika zoezi la kuuaga miili 13 ya watu waliokufa baada ya kuangukiwa na jengo katika eneo la Kariakoo siku ya Jumamosi, Novemba 16.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema hafla hiyo itafanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia saa saba mchana leo Novemba 18.

Watu 13 wamethibitika kuaga dunia na makumi wengine kunusurika baada ya jengo la ghorofa nne kuporomoka katika eneo lenye wafanyabiashara wengi jijini Dar es Salaam.

Advertisement

Waziri Mkuu ambaye alifika katika eneo hilo kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan aliwataka wananchi kuwa na subira wakati vyombo vya uokoaji vikiendelea na kazi yake.