Walionyongwa waongezeka kwa asilimia 53

SHIRIKA la Kimataifa la Kutetea Haki za Binaadamu ‘ Amnesty International’ limesema idadi ya watu waliouawa kwa kunyongwa ulimwenguni kote mwaka 2022, imeongezeka kwa asilimia 53. Limeeleza shirika hilo katika ripoti yake.

Shirika hilo limesema kuwa jumla ya watu 883 waliuawa katika nchi 20, na kuashiria kupanda kwa 53% zaidi ya 2021, ripoti hiyo halijumuishi maelfu ya watu wanaoaminika kutekelezwa nchini China mwaka 2022. Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, ambapo takwimu zilizorekodiwa zilipanda kutoka 520 mwaka 2021 hadi 825 mwaka 2022.

Amnesty imesema idadi hiyo imefikia watu 883. Hiyo ni idadi ya juu zaidi ya matukio hayo tangu mwaka 2017. Taarifa hiyo imetupia lawama mataifa ya Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika, ikiwa ni pamoja na Iran, Saudi Arabia na Misri, ambayo yanafahamika kwa kutekeleza adhabu ya kifo.

“Nchi za Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini zilikiuka sheria za kimataifa huku zikiongeza mauaji mwaka wa 2022, na kufichua kutojali maisha ya binadamu. Idadi ya watu walionyimwa maisha iliongezeka sana katika eneo lote; Saudi Arabia iliwanyonga watu 81 kwa siku moja,”

“Hivi majuzi, katika jaribio la kukata tamaa la kukomesha uasi wa wananchi, Iran iliwanyonga watu kwa sababu tu ya kutumia haki yao ya kuandamana,” Agnès Callamard, Katibu Mkuu wa Amnesty International alisema katika taarifa hiyo.”

Aidha ripoti inaonesha 90% ya hukumu zinazojulikana duniani nje ya Uchina zilitekelezwa na nchi tatu tu katika eneo hilo. Idadi ya watu walionyongwa nchini Iran iliongezeka kutoka 314 mwaka 2021 hadi 576 mwaka 2022; Idadi hiyo iliongezeka mara tatu nchini Saudi Arabia, kutoka 65 mwaka 2021 hadi 196 mwaka 2022 dadi kubwa zaidi iliyorekodiwa na Amnesty katika miaka 30 wakati Misri iliwanyonga watu 24.

Ripoti hiyo imebaini kuwa usiri wa serikali za Korea Kaskazini na Vietnam pamoja na upatikanaji duni wa taarifa katika nchi kadhaa, vinazuia utoaji wa tathmini kamili ya hukumu ya vifo.

Habari Zifananazo

Back to top button