Walioshambulia waandishi Ngorongoro kusakwa

ARUSHA: MKUU wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amelaani tukio la wanahabari kushambuliwa na kujeruhiwa na baadhi ya vijana jamii ya kifugaji walipokuwa wakitekeleza majukumu yao eneo la Enduleni ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngororongoro (NCAA).

Kutokana na hali hiyo ameliagiza jeshi la Polisi kukamata watuhumiwa hao na sheria kuchukua mkondo wake bila kujali muhusika ana wadhifa gani.

Akizungumza wakati alipotembelea hospitali ya Fame iliyopo wilayani Karatu, amesema wanahabari hao walikuwa wakitekeleza majukumu yao juzi ya kuzungumza na wafugaji walioamua kuhama kwa hiari kupisha uhifadhi.

Amesema, serikali itawasaka wahusika na kuwachukulia hatua na kwamba mhusika kama ni Mbunge, diwani au wadhifa mwingine wowote atakamatwa tu.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,Justine Masejo amesema jeshi la polisi tayari limeshafungua jalada la shauri hilo na wanaendelea na upelelezi wa tukio hilo

Awali Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Elibariki Bajuta alisema NCAA imesikitishwa na tukio hilo na kutoa rai kwa wanasiasa kuacha uchochezi.

Habari Zifananazo

Back to top button