Wamiliki vituo vya kulea watoto mchana watakiwa kufuata miongozo

VITUO vya kulea watoto mchana ‘daycare center’ vinashindwa kujipambanua vyema ili kuendana na matakwa ya sheria,sera na muongozo dhidi ya kumlinda mtoto.

Sheria hizo mojawapo ni sheria ya mtoto namba 21 ya mwaka 2009 iliyofanyiwa maboresho mwaka 2019 na muongozo uliopo juu uendeshaji wa vituo hivyo ili viendane na sifa stahiki za ukuaji timilifu kwa mtoto.

Wazazi wamekuwa wakiamini vituo vya kulelea watoto kwa asilimia 100 lakini mamlaka za usimamizi zinapochukua jukumu ya kuzikagua zimekuwa zikikuta dosari nyingi mojawapo kukosa usajili na mazingira mabovu.

Samson Gasomi na Hadija Mliwa wakazi wa manispaa ya Shinyanga wanasema changamoto ya uanzishwaji wa vituo vya kulelea watoto mchana mojawapo ni wamiliki kuvianzisha kinyemelea bila kuwa na uelewa wakutosha kuhusu muongozo.

Gasomi anasema huenda usajili unapatikana kwa ugumu au usumbufu ndiyo maana wanaamua kuanzisha hivyo hivyo sababu tayari wana maono katika malengo yao.

“Tunapenda wazazi nao waelimishwe kuwa mtoto wa miaka miwli hadi mitano akienda kwenye vituo vya kulelea watoto sio kuandika bali ni kuimba na kucheza ilia pate uchangamfu”anasema Gasomi.

Mmoja wa Wamiliki kutoka kituo cha kulelea watoto mchana ambacho hakina usajili jina limehifadhiwa anasema wazazi wanapenda watoto wao wafundishwe kuandika lakini usipofanya hivyo kesho wanahamisha mtoto wao.

Katibu msaidizi wa Umoja wa Wamiliki wa Vituo vya Kulelea Watoto Wadogo Mchana Olivia Maganga ambaye pia Mmiliki wa kituo cha Goshen anasema wanaomba muda ili waweze kujipanga kuweza kusajili .

Maganga anasema kituo chake hakina usajili ambapo anasema wapewe muda wa kuboresha mazingira na kuanza taratibu za usajili kwa kufuata miongozo na sheria na kanuni.

Ofisa ustawi wa jamii kutoka mkoani Shinyanga Lyidia Kwesigabo anasema katika ufuatliaji amebaini (daycare center) 52 mkoani Shinyanga zinajiendesha bila usajili.

Kwesigabo anasema amechukua jukumu la kwanza kuomba viongozi kwenye ngazi za halmashauri kuisaidia kutoa elimu ili wamiliki wa vituo hivyo waweze kufuata Sheria na muongozo uliowekwa.

Kwesigabo anasema kuna vituo 96 vya kulelea watoto mchana lakini vilivyosajiliwa ni 44 tu na zoezi la kuvifungia visivyo na sifa litaanza mwezi Januari ambapo vituo vyote vitajipanga kuanza kutoa huduma.

Kwesigabo anasema usajili wa vituo hivyo unasimamiwa na kamishna wa ustawi wa jamii na vinatakiwa kufuata muongozo wa uanzishaji wa vituo,Sheria ya namba 21 ya mwaka 2009 iliyofanyiwa maboresho mwaka 2019.

Kwesigabo anasema halmashauri ya manispaa ya Kahama imejitahidi vituo vyake vyote 20 kuvisajili , halmashauri ya Msalala kati ya vituo sita kimoja ndiyo kimesajiliwa na halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga vituo 41 lakini vituo 19 tu ndiyo vimesajiliwa.

“Leo nimesimama hapa kuomba kusaidiana kulea watoto wetu kupitia pia vituo vya kulelea watoto mchana kwani vimegubikwa na changamoto nyingi ikiwemo mazingira mabovu mfano kisima kuchimbwa karibu na maeneo ya kuchezea watoto”anasema Kwesigabo.

Kwesigabo anasema baadhi ya vituo vimekuwa na visima visivyofunikwa pamoja na kutotoa lishe bora kwa watoto,ufundishaji wa watoto kwa kuandika kinyume na muongozo unavyotaka mtoto apate uchangamfu kwa kuimba nyimbo za ujumbe mbalimbali.

“Muongozo uliopo kwanza yawepo mazingira mazuri kwa mtoto kwa kucheza,anayewafundisha awe na ujuzi na ubunifu ,kuwepo vyoo bora,lishe bora na eneo la kupumzikia”anasema Kwesigabo.

Kwesigabo anasema vituo pia vinatakiwa kufuata Sera ya Afya ya mwaka 2007 ndiyo maana wataalamu wa afya wanahusika kukagua maeneo ya vituo ili kuona kama yamekidhi matakwa ya Sera na Muongozo wa uanzishaji wa vituo.

Kwesigabo anasema katika Programu Jumuishi ya Tataifa ya Makuzi, Malezi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto( PJT-MMMAM) yanahitaji mtoto kupatiwa nguzo tano muhimu ambazo ni lishe Bora,afya,ujifunzaji wa awali,.malezi yenye mwitikio na ulinzi na Usalama hata akiwa kwenye vituo hivyo.

“Kipindi cha mwezi Januari mwaka 2024 tunaomba vituo vifuate utaratibu uliowekwa na kufuata nguzo tano kwa mtoto ili aendelee kupata ukuaji uliotimilifu”anasema Kwesigabo.

Kaimu mganga mkuu wa mkoa Dkt Nuru Mpuya anasema kumekuwepo na uholela wa uanzishaji wa vituo hivi pasipo kufuata sheria,taratibu na miongozo hivyo kuanzia leo wamiliki wafanye usajili na baada ya muda uliopangwa timu itapita kukagua na kujirizisha kama utaratibu ulifuatwa.

“Tunataka vituo vyote viwe vimesajiliwa na tukikuta mmiliki hujasajili hatua zitachukuliwa za kisheria kwa kutozwa faini,pia wamiliki wote wawe wanawasilisha ripoti zao kwa maafisa ustawi katika halmashauri”anasema dk Mpuya.

.Kaimu ofisa Elimu mkoa Dedan Rutabazi anasema malalamiko kwa wakaguzi na uthibiti ubora wa shule kuwafungia yamekuwepo kwani wamekuwa wakikiuka taratibu wanafundisha kwenye vituo vyao badala ya kutoa elimu changamshi.

Kamishna msaidizi idara ya ustawi wa jamii kutoka ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa Amoni M Paju anasema vituo vya kulelea watoto mchana vinatakiwa kufuata muongozo ili watoto wapate makuzi na malezi bora katika ukuaji wao.

“Ili kufikia ukuaji wenye utimilifu watoto wawe kwenye mazingira bora y kwani ukianza kumfundisha mtoto nne ongeza nne ubongo wake bado haujakomaa hapo unampoteza”anasema Mpaju.

Habari Zifananazo

Back to top button