JUMLA ya Wananchi 250,000 wa Wilaya ya Muleba wanatarajia kushiriki zoezi la uandikishaji wa orodha ya wapiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaaa na vijiji utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu.
Msimamizi wa uchaguzi wa wilaya hiyo, Issaya Mbenje amefanya zoezi la kutembelea vituo mbalimbali vya uandikishaji na kuzunguma na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa wilaya hiyo Ina kata 43 na vijiji 166 huku vituo vilivyotenga kuboresha daftari la uboreshaji ni 802.
Amesema mpaka sasa maandalizi yamekamilika na vituo vyote vimefunguliwa huku akitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha ili kupata haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi watakaowaletea maendeleo.
SOMA: Watakiwa wasijichukulie sheria mkononi
Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Dk Abel Nyamahanga amesema kuwa anatambua kuwa Wilaya ya Muleba imezungukwa na visiwan vingi hivyo ametoa wito kwa ambao sio wakazi wasishiriki zoezi Hilo kwani zoezi Hilo linawahusu wakazi wenyewe wa eneo hilo kwenye vitongoji na vijiji husika.
“Tunawingi wa visiwan na maeneo yetu kunawafanyabishara wengi wanakuja katika visiwa vyetu , tunahamasisha shughuli ziendelee lakini kama sio mtanzania kama sio mkazi usidhubutu kujiandikisha katika daftari au kushiriki uchaguzi huo,” amesema Dk Nyamahanga.
Jilala Chobo mwananchi wa kitongoji Bugombe Wilaya ya Muleba amesema ili wananchi wawapate viongozi wanaotaka wanapaswa kujitokeza kwa wingi na kujiandikisha katika daftari la uchaguzi kwani maamuzi pekee ya kumpata kiongozi wa kweli ni kujiandikisha ili usubiri kupiga kura.
Wakala wa Chama Cha Siasa, Hassan Ayub akiwa katika kituo cha uandikishaji cha kijiji Magata alipongeza utaratibu uliowekwa na serikali katika maswala ya uandikishaji kwa kuhakikisha kila mwenye haki ya kujiandikisha anapata fursa ya kujiandikisha bila kubuguziwa.