Wanafunzi Arusha wafundwa athari dawa za kulevya

MAMLAKA ya Kudhiti na Kupambana na Dawa za Kulevya(DCEA)Kanda ya Kaskazini pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Arusha wametoa elimu kwa wanafunzi zaidi ya 547 wa shule ya sekondari ili wasijiingize kwenye matumizi ya dawa za kulevya na kutimiza ndoto zao.

Akizungumzia lengo la mafunzo hayo ya siku moja yaliyotolewa  na Chuo Cha Uhasibu Arusha (IAA), Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Arusha, Zawadi Ngailo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amesema watoto wakike wanakumbana na changamoto mbalimbali hivyo wanashirikiana na DCEA kwa pamoja kutoa elimu ya rushwa na upingaji wa matumizi ya dawa za kulevya

Ngailo amesema watoto wa kike lazima wapewe mbinu za kukataa rushwa zozote ikiwemo rushwa ya ngono na kutoa taarifa sehemu husika ili hatua zichukuliwe kwani endapo rushwa ikifumbiwa macho itaweza kuleta maafa makubwa kwa jamii ikiwemo dawa za kulevya .

“Tuone taarifa za rushwa sanjari na matumizi ya dawa za kulevya popote pale mnapokumbana na changamoto haswa nyie wanafunzi,lakini pia muhakikishe mnatimiza ndoto zenu kwa kutojiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya”

Ofisa Elimu Jamii kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Kanda ya Kaskazini(DCEA) Shabani Miraji amesema mamlaka hiyo , Takukuru na waliokuwa watumiaji wa dawa hizo (waraibu ) wametoa elimu ya pamoja ili kuwasaidia wanafunzi wakike kutojiingiza katika matumizi ya dawa hizo pamoja na suala zima la rushwa.

Habari Zifananazo

Back to top button