Wanafunzi Bwiru watwaa tuzo wanasayansi chipukizi

WANAFUNZI wa shule ya sekondari ya wanaume ya Bwiru, iliyoko jijini Mwanza wameibuka washindi wa jumla katika tuzo za wanasayansi chipukizi (YST) baada ya kuandika mradi unaohusu tathmini ya kiwango cha usafi wa maji katika shule za sekondari.

Washindi hao ni miongoni mwa wanafunzi 90 kutoka mikoa yote Tanzania walioonesha kazi zao za ugunduzi wa Sayansi na Teknolojia Dar es Salaam

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu ch Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) Profesa Bruno Sunguya alikabidhi tuzo hizo kwa washindi, akimwakilisha Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda, katika shindano lililoandaliwa na Taasisi ya Wanasayansi Chipukizi (YST).

Katika shindano hilo jumla ya kazi za kigunduzi wa kisayansi zipatazo 45 ziliwasilishwa na wanafunzi wa shule hizo za sekondari kutoka Tanzania Bara na Visiwani.

Wakizungumzia mradi uliowapa ushindi kwa nyakati tofauti ,Anord Philip na Ernest Emilly walisema mada hiyo inatokana na kuwepo kwa tatizo la magonjwa ya mara kwa mara ya tumbo, amiba kwa wanafunzi wa shule za bweni , hivyo kuhitaji kujua kiwango cha usafi na usalama wake.

Akizungumza Profesa Mkenda amesema tuzo hizo kwa wanafunzi zinasaidia kuhamasisha masomo ya Sayansi katika kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

Amewataka wanafunzi kuendelea kusoma kwa bidii na kuongeza ubunifu katika nyanja mbalimbali kwani ni eneo linaliweza kuonesha vipaji vyao.

“Bunifu zinazoibuliwa na wanafunzi hawa ni zile zinazoendelea kutoa suluhu kwa matatizo ya kila siku yanayoikabili jamii,” amesema Profesa Mkenda na kuongeza kuwa mawazo ya kibunifu ya sayansi yanasaidia kujenga nchi kwa vizazi vijavyo.

Amesema maonesho hayo yanahamasisha masomo ya Sayansi mashuleni katika kuleta mabadiliko nchini. Mbali ya tuzo wazipatazo wanafunzi lakini washindi hupata udhamini wa kusoma masomo ya elimu ya juu bure kupitia Karimjee Foundation

Habari Zifananazo

Back to top button