Wanafunzi Kiyanga wafundwa kuhusu masomo

MBUNGE wa Jimbo la Nanyamba mkoani Mtwara Abdallah Chikota amewataka wanafunzi katika Shule ya Sekondari ya Kiyanga iliyopo kata ya Kiyanga Halmashauri ya Mji Nanyamba kuhakikisha wanajiwekea malengo katika elimu yao ili aweze kufika kidato cha nne na zaidi.

Akizungumza leo mkoani Mtwara alipotembelea shule hiyo ya sekondari ya kiyanga kwenye halmashauri hiyo, Chikota amesema wanafunzi hao wanapoanza elimu hiyo ya kidato cha kwanza wawejiwekee malengo ya kusoma ili wafike mbali zaidi kielimu ikiwemo elimu ya juu.

Adha shule hiyo ni mpya ambayo imenza rasmi Februari 2025 yenye mkondo mmoja wa kidato cha kwanza, mradi wenye vyumba vinne vya madarasa na matundu kumi ya vyoo uliyogharimu zaidi Sh milioni 80.

“Mnaanza hapa kusoma leo, mjiwekee malengo ya kosoma ili muweze kuhitimu mufike kidato cha nne, kidato cha sita kisha elimu ya chuo kikuu”

Amesema serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeshalifanyia kazi suala la upungufu wa miundombinu ya sekondari hiyo ambapo imetenga fedha zaidi ya Sh milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya shule hiyo.

“Niwasihi, kuna watu walikuwa wanabeza sekondari za kata lakini sekondari za kata sasa hivi kutokana na uwekezaji mkubwa ambao umefanywa na serikali yetu watoto wanafanya vizuri”amesema Chikota.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Vagrey Kidava amesema shule inatarajiwa kupokea wanafunzi 86 wa kidato cha kwanza mwaka huu ambapo mpaka sasa wanafunzi 75 wamesharipoti.

Aidha amezitaja faida za kuwepo kwa mradi huo kwenye kata hiyo ikiwemo kuwapunguzia wazazi mzigo wa gharama za kuwahudumia wanafunzi kutokana na shule kuwa karibu na maeneo wanayoishi.

Licha ya faida hizo lakini shule inakabiliwa na baadha ya changamoto ikiwemo ukosefu wa nyumba za walimu, nishati ya umeme, kisima cha kuvunia maji ya mvua na zingine.

Kwa Upande wao baadhi ya wanafunzi shuleni hapo akiwemo Sarah Abdallah ameipongeza serikali kwa kuwajengea shule hiyo kwenye maeneo yao huku akiahidi kusoma kwa bidii ili aweze kufikia ndoto zake.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button