Wanafunzi kunufaika na programu zenye tija

KATIBU Mtendaji wa NACTVET, Dk Adolf Rutayuga amewataka wakuu wa vyuo binafsi vya elimu na mafunzo ya ufundi stadi kuanzisha programu zinazokidhi mahitaji mbalimbali kwenye jamii.

Dk Rutayuga amesema hayo wakati wa ufunguzi wa awamu ya pili ya mafunzo kwa wamiliki na wakuu wa vyuo binafsi vya mafunzo ya ufundi stadi kutoka Kanda ya Kusini na Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yaliyofanyika mkoani Morogoro.

Mafunzo hayo yanalengo la kuwajengea uwezo wakuu na wamiliki wa vyuo binafsi katika utoaji wa mafunzo ili kusaidia katika kukidhi mahitaji ya jamii na kutoa wataalam wenye ujuzi na umahiri.

Ameongeza kuwa, nia ya baraza ni kuvisaidia na kuvilea vyuo hivyo ili viweze kufikia malengo huku akiwasihi wamiliki/wakuu wa vyuo kufuata sheria, kanuni na taratibu za NACTVET ikiwa ni pamoja na kufanyia kazi mapungufu yaliyoainishwa vyuoni mwao ili kuendana na ubora unaohitajika.

Mkurugenzi wa Quality Development College,  Nurudini Nhuva kwa niaba ya washiriki, amepongeza NACTVET kwa kuandaa mafunzo hayo yaliyowaleta pamoja na kusikiliza changamoto zao kwa maendeleo ya Elimu ya Ufundi Stadi nchini huku akiwashauri washiriki wengine kufuata Kanuni na taratibu zilizowekwa na NACTVET.

Miongoni mwa watumishi wa NACTVET walioshiriki katika kutoa mafunzo hayo ni pamoja na Dk,Alex Nkondola, Mkurugenzi(Huduma za Taasisi), Dk Amani Makota, Mkurugenzi (Huduma za uendeshaji vyuo) Dk Hirst Ndisa (Meneja Kanda ya kusini)

Baraza hiyo linajumla ya vyuo 1329 (VET- 805, TET- 465, FDC- 55) vya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi inavyovisimamia nchini.

Habari Zifananazo

Back to top button