HONG KONG : WANAHARAKATI mashuhuri 45 kati 47 wamehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela baada ya kukutwa na hatia ya kufanya kosa la uasi nchini humo.
Hatua hii imechukuliwa baada ya wanaharakati hao kukutwa na hatia ya kuhatarisha usalama wa taifa.
Washtakiwa hawa walifunguliwa mashtaka mwaka 2021 ambao walikabiliana na kifungo cha maisha jela chini ya sheria kali iliyowekwa na Beijing na iliyokandamiza vuguvugu la kuunga mkono demokrasia ambayo ilijizolea umaarufu mkubwa.
Hata hivyo washtakiwa 45 walikiri kufanya makosa lakini wengine wawili wameachiliwa huru.
Wakatihuohuo waangalizi wa masuala ya sheria nchini humo wamesema mamlaka za serikali nchini humo zimekuwa zikikandamiza upinzani wa vyombo vya habari kufuatia maandamano makubwa dhidi ya serikali ya mwaka 2019.