Wananchi 2000 waondokana na changamoto ya maji Kilindi

TANGA, Kilindi: Zaidi ya wananchi 2800 waliopo Kijiji cha Ngobole kata ya Saunyi wilayani Kilindi wameondokana na adha ya maji iliyokuwa ikiwakabili muda mrefu baada ya kukamilika kwa mradi wa maji wenye thamani ya zaidi ya sh Mil 259.2.
Mradi huo ambao umetekelezwa na Shirika la World Vision umeweza kuwasaidia wananchi hao kupunguza adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo.
Akiongea na wananchi hao Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Hashim Mgandilwa amesema kuwa Wilaya hiyo inakabiliwa na uhitaji mkubwa wa huduma ya maji kwani mpaka sasa wamefikia asilimia 35 tu.
“Dhamira ya serikali ni kuhakikisha Halmashauri za Wilaya ziweze kufikisha asilimia 85 ya upatikanaji wa huduma ya maji ifikapo 2025 na Kilindi ni Wilaya ambayo bado ina uhitaji mkubwa wa huduma hiyo” amesema DC Mgandilwa.
 
Naye Mratibu wa mradi wa Mgera AP Modestus Kessy amesema kuwa kukamilika Kwa mradi huo utasaidia kuondoa adha ya kutumia huduma ya maji baina ya wananchi na mifugo.
 
“Tayari miradi kama hii imeshafanyika katika maeneo mengi kwenye wilaya hii lengo ikiwa ni kuunga jitihada za serikali za kuwasogezea huduma wananchi wake”amesema Kessy.
4 comments

Comments are closed.