Wananchi 367 hawama Ngorongoro

MUITIKIO wa wananchi wanaoishi katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kuendelea kuhama kwa hiari umekuwa mkubwa baada ya leo jumla ya kaya 79 zenye watu 367 na mifugo 995 kuhama kutoka hifadhi hiyo kwenda kijiji cha Msomera wilayani Handeni mkoani Tanga na maeneo mengine waliyochagua wenyewe.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii (anayesimamia maliasili), Benedict Wakulyamba amesema kuwa kuondoka kwa kundi hilo ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa kulinusuru eneo la Hifadhi ya Ngorongoro ambapo wananchi wanapewa elimu ya kuhama  kwa hiari ili kuboresha maisha yao na kunufaika na fursa za kiuchumi zilizoko nje ya hifadhi.

SOMA: Serikali yatoa tamko, kuhamisha wananchi Ngorongoro

Wakulyamba amewasisitizia wananchi hao kuwa mabalozi wa kazi nzuri iliyofanywa na serikali katika kuboresha huduma za kijamii na fursa za kiuchumi katika kijiji hicho na kuwafahamisha wenzao waliobaki wajue fursa hizo na kuhamasika kuhama.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by HABARILEO (@habarileo_tz)

Pia ametoa tahadhari kwa baadhi ya wananchi ambao wamekuwa wakihamia Msomera kinyemela bila kufuata utaratibu uliowekwa na hivyo kuleta changamoto kwa ndugu zao wanaowakuta huko na kuwasihi kuwa kufuata utaratibu na miongozo iliyowekwa ili wawe wakazi halali katika maeneo wanayopenda kuhamia.

SOMA: Waliogoma kuhama Ngorongoro wajuta

Ofisa Uhifadhi mkuu na Meneja mradi wa kuhamisha wananchi kwa hiari (PCO), Flora Assey amebainisha kuwa tangu zoezi hilo lilipoanza Juni, 2022 hadi kufikia Agosti, 2024 takriban kaya 1,598 zenye watu 9,618 na mifugo 39,779 imeshahama ndani ya hifadhi kwenda Kijiji cha Msomera na maeneo mengine.

Habari Zifananazo

Back to top button