Wananchi Esilalei, Losirwa kunufaika mradi wa maji

ARUSHA: WANANCHI zaidi ya 8,757 kutoka vijiji vya Esilalei, Losirwa wamenufaika na mradi wa maji wilayani Monduli mkoani Arusha.
Hayo yamesemwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Ismail Ali Ussi wakati wa kuzindua mradi wa maji kutoka kwa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) uliogharimu Sh bilioni 1.9
Amesema mwenge huo wa uhuru umewapa matumaini wananchi hao katika kuhakikisha maji yanapatikana karibu na makazi yao.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete amempongeza Rais Samia Hassan Suluhu kwa kutatua kero ya maji ambao ilikuwa ni ya muda mrefu wilayani Monduli kwakuhakikisha wananchi wanapata maji na kumpongeza aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Fredy Lowassa kwa kuhakikisha Monduli inapata maendeleo.
SOMA ZAIDI

Awali akisoma taarifa ya mradi huo Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini(RUWASA) wilaya ya Monduli, Mhandisi Neville Msaki amesema mradi huo umegharimu kiasi cha sh, bilioni 1.9 na utahudumia wananchi 8,757 kutoka vijiji vya Eslalei,Losirwa na wengine ikiwemo mifugo 26,400 kupata maji ya kunywa”.



