Mwenge wazindua miradi ya bil 30/- Arusha

ARUSHA: MWENGE wa Uhuru wawasili mkoani Arusha na kuzindua miradi 54 yenye thamani ya Sh bilioni 30.3 katika halmashauri saba za mkoa huu.
Mwenge huo umewasili leo mkoani hapa na kukabithiwa eneo la King’ori Kibaoni wilayani Arumeru na kukabithiwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Kenan Kihongosi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu.
Mara baada ya kupokea mwenge huo, RC Kihongosi amesema mwenge huo utakimbizwa umbali wa kilomita 1,203.17 kwenye wilaya sita na halmashauri saba za Mkoa wa Arusha na kupitia jumla ya miradi 54 kisekta yenye thamani ya Sh bilioni 30.3.
SOMA ZAIDI
Aidha, katika miradi hiyo 54, miradi 18 yenye thamani ya Sh bilioni 12 itawekewa mawe ya msingi, miradi minne yenye thamani ya Sh milioni 378.2 itafunguliwa, miradi 19 yenye thamani ya Sh bilioni 15.2 itazinduliwa na miradi 13 yenye thamani ya Sh bilioni 2.6 itatembelewa.