Wananchi kufundishwa kuishi na wanyama

DAR ES SALAAM; CHUO Kikuu cha Dar es Salaam ( UDSM), kimepeleka wataalamU kwenye mikoa miwili kwa ajili ya kuwafundisha wananchi namna ya kuishi na wanyama wakali, kwa kuweka vitu vitakavyowafanya wasisogelee mashamba na makazi yao.

Ofisa Mradi wa Ushirikiano kati ya Vyuo Vikuu, Mary Malekela amesema hayo wakati wa maonesho ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Advertisement

 

Malekela amesema wataalamu hao walipelekwa katika Wilaya ya Monduli, Kijiji cha Naitoria na Mkoa wa Lindi Kijiji cha Mlola kwa kuwa maeneo hayo ni njia za wanyama hususani tembo.

Soma pia:https://habarileo.co.tz/tawa-kuimarisha-ulinzi-wa-wananchi-dhidi-ya-wanyamapori/

Amesema mafunzo hayo ni muhimu kwa sababu, imewahi kutokea mwanamke mmoja aliuawa baada ya kuona tembo na kupiga kelele, huku wale waliokuwa kimya hawakudhuriwa.

Amesema mradi huo unahusisha Chuo Kikuu Michigan kilichopo Marekani, UDSM, Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam ( DUCE) pamoja na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo ( SUA), kilichopo Morogoro. Pia wanashirikiana Manispaa ya Lindi na Halmashauri ya Monduli.

Amesema mradi huo unajishughulisha na shughuli za maendeleo katika sekta ya elimu, afya, maji, kilimo na kujengea uwezo wananchi.