Wananchi Kyerwa wasogezewa karibu kuduma za kisheria

Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila akiapisha

Wananchi wa wilaya ya Kyerwa wanatarajia kupunguza mwendo wa kilometa 100 ambao walikuwa wakitembea kutoka Kyerwa hadi Karagwe kwa ajili ya kufata huduma za kisheria katika maswala ya ardhi.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Alberth Chalamila amewaapisha wajumbe wa Baraza la Ardhi katika wilaya ya Kyerwa ikiwa ni miaka mingi tangu Wilaya hiyo kuwepo bila kuwa na huduma yeyote ya kisheria katika maswala ya ardhi.

Wajumbe wa Baraza la Ardhi ambao wanateuliwa na waziri wa Ardhi ,Nyumba na makazi walioapishwa ni Elias Titilindwa ,Ezra Rugakira,na Esta mtafuta ambao watahudumu katika Baraza la Ardhi chini ya mwenyekiti wa Baraza la Ardhi la Karagwe David Simon kwa kipindi Cha miaka mitatu.

Advertisement

Katika uapisho huo mkuu wa mkoa wa Kagera alisema asilimia 80 ya migogoro iliyopo mkoani Kagera inachangiwa na migogoro ya Ardhi hivyo anatumaini kwamba uwepo wa Baraza Hilo utapunguza kero katika wilaya ya Kyerwa pamoja na kuleta matumaini mapya juu ya waliokosa haki katika maswala ya Ardhi.

“Kama angekuwepo kamanda wa polisi mkoani Kagera mungeona Ni kwa jinsi gani migogoro ya Ardhi inachangia watu kuuana ,lakini pia mkoa huu ndo mkoa ambao kitu kidogo tu tayari mtu amekimbilia mahakamani wengi hawataki Suluhu ya wenyewe kwa wenyewe ,nawaomba Kama mabaraza punguzeni maswala ya migogoro mtawaliwe na Hekima na kujiepusha na Rushwa mkitenda haki kwa sababu mmeaminiwa na serikali kesi au migogoro haitachelewa”alisema Chalamila.

Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Rashid Mwaimu alisema kuwa amekuwa akipokea Kero za Ardhi katika wilaya ya Kyerwa na kero kubwa Ni umbali ulipo kutoka Kyerwa kwenda Karagwe kwa kilometa zaidi ya 100 ili kuhudhulia kesi zao.

Alisema anaamini kuwa uwepo wa Baraza la Ardhi utarahisisha umalizikaji wa mashauri mengi ya Ardhi yaliyopo ambayo yanasubiri kupata ufumbuzi wa haraka.

Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi Wilaya ya Karagwe David Simoni ambaye anatarajia kuhudumu Kama mwenyekiti wa Baraza la Ardhi Kyerwa alisema kuwa amekuwa akishuhudia wanaodai haki wakitumi gharama za kulala ili kuwai mashauri Yao na kupata haki.

Alisema Kuna muda kesi ambayo inapaswakumalizika ndani ya muda mfupi inachukua hata miaka mitano kutokana na mshitakiwa au anayeshitaki kukosa uwezo wa kuhudhulia mahakamani kutokana na umbali mrefu.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *