Wananchi Shinyanga wajitokeza kupiga kura

WANANCHI Manispaa ya Shinyanga wamejitokeza katika kupiga kura za kuwachagua viongozi wa Serikali za Mtaa huku wakitakiwa kulinda amani kwa kuwa watulivu.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha amesema hayo leo wakati wa zoezi la upigaji kura kwenye Mtaa wa Mkuu wa Mkoa Lubaga na zoezi likiendelea nakuwataka wanapomaliza kupiga kura warudi nyumbani wasubiri matokea.

Advertisement

Macha amesema hofu iliyopo ilikuwa ni mvua lakini dalili ya hali ya hewa hali ni shwari.

Mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Jackosni Myawami amesema ipo changamoto ya watu kukosa majina yao kwenye vituo vya wazi nakuomba msimamizi aweze kuliangalia hilo.

Msimamizi wa uchaguzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga my Alexius Kagunze amesema tayari vituo vimefunguliwa saa mbili asubuhi na mawakala wako kwenye vituo na wananchi wameanza kujitokeza.

“Tunategemea wananchi 120,000 wajitokeze kupiga kura na vituo vilivyopo ni 285 kati ya hivyo vituo 149 vya wazi na vingine vipo kwenye majengo ya Umma,” amesema Kagunze.