Wananchi Tungli wahaha huduma ya afya
ZAIDI ya wakazi 7,000 katika kijiji cha Tungli wilayani Kilindi mkoani Tanga wanalazimika kutembea umbali wa Km 90 kufuata huduma ya afya kutokana na ukosefu wa kituo cha afa licha ya serikali kupeleka Sh milioni 400.
Uwepo wa vifo vya wajawazito ni miongoni mwa changamoto ambazo zinawakabili wananchi wa eneo hilo hatua ambayo inawalazimu kwenda katika wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro kuweza kupata huduma hiyo.
Hati hiyo imemshangaza Mwenyekiti wa Chama Chama Mainduzi Mkoa wa Tanga, Rajab Abdulrahaman baada ya kukuta magofu ya majengo ya kituo hicho yakiwa hayajakamilika licha ya serikali kupeleka fedha kwa ajili ya umaliziaji wa kituo hicho ili kiweze kutoa huduma kwa wananchi.
“Serikali imeleta fedha muda mrefu katika eneo hili toka mwaka 2021 mpaka leo haijamalizika huu ni ujanja ujanja ninaouona hapa Mkuu wa wilaya hawa watu chama kilikuja hapa kuomba ridhaa ya kuongoza na kuweka ahadi ya kujenga kituo cha afya ambacho mpaka leo hakijakamilika”alisema mwenyekiti huyo.