“Wananchi wachague viongozi wa CCM”

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM ) John Mongella amewataka wananchi wachague viongozi wanaotokana na chama hicho ili maendeleo yaweze kuja kwa haraka.

Mongella amesema hayo leo mjini Shinyanga alipowasili kwaajili ya kufunga Kampeni ya uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo mkutano umeandaliwa kata ya Kitangili.

Mongella amesema leo ni mwisho wa kampeni wananchi wajitokeze kupiga kura kwa usahihi nakukipa chama ushindi kwa kuchagua viongozi wanaotokana na chama hicho.

Advertisement

katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga Odilia Batimayo amesema jimbo la Wilaya ya Shibyanga mjini lina mitaa 35 ambapo yote wanamatumaini ya kupata ushindi.