Wananchi waililia CCM mmomonyoko wa maadili

WANANCHI wa Kijiji cha Mtinko wilayani Singida serikali iingilie kati mmomonyoko wa maadili katika jamii unaofanya baadhi ya wananchi kuvaa mavazi yasiyo na staa na kutembea uchi kinyume na mila,desturi na utamaduni wa Mtanzania.

Ombi hilo wamelitoa leo katika mkutano wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Daniel Chongolo aliyeambatana na kamati ya sekretarieti ya chama kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM 2020/25 na kukagua uhai wa mashina.

Akizungumza kero hiyo mmoja wa wanakijiji hao alisema maadili hivi sasa yameporomoka na baadhi ya wananchi wanatembea uchi kinyume na maadili ya mtanzania.

Chongolo amesema wazazi na walezi wamesahau kazi yao ya maadili kwa watoto na hali hiyo imefanya kuwepo na kuporomoka kwa maadili.

“Malezi kwetu wazazi yameanza kuporomoka,tumeacha kuwalea watoto wetu,lazima tubadilike,tulinde utamaduni wa maadili yetu,tusiache wafanya mambo yanayotudhalilisha,”amesema Chongolo.

Habari Zifananazo

Back to top button