Wananchi wamshukuru Samia kampeni msaada wa kisheria

ARUSHA: WANANCHI wanaoendelea kupata msaada wa kisheria kupitia kampeni ya ‘Mama Samia Legal Aid Campaign’ mkoani Arusha wamemshukuu Rais Samia Hassan Suluhu na Wizara ya Katiba na Sheria kwa kuwezesha wataalam wa sheria kusikiliza migogoro ya kifamilia.

Pongezi hizo zimetolewa leo na wananchi hao akiwemo Asma Juma na Shukrani Mohamed wanaoendelea kumiminika katika banda hilo kwaaajili ya kupata ufumbuzi wa madai mbalimbali ya kisheria.

Shukrani amesema amefika bandani hapo akiwa na changamoto ya ardhi baada ya eneo lake kuuzwa kwa mara ya pili na mhusika lakini kupitia mawakili hao mhusika ameweza kuitwa na kukiri ni kweli ameuza eneo hilo kisha kumrejeshea eneo lake halali lililouzwa marbili.

“Hii kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia  Legal Aid ya  kutatua changamoto zilizoshindikana na kupata ufumbuzi iendelee na tunamshukuru Rais Samia kwa kuileta sisi wananchi wanyonge tunanufaika”

Naye Asma amesisitiza wananchi wengine kutumia huduma hiyo ili waweze kunufaika nayo ikiwemo kupunguza kesi mahakamani zinazoweza kutatuliwa kupitia kampeni hiyo

Kampeni hiyo inaendelea kutolewa ikiwa ni wiki ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani itakayofanyika Machi 8, 2025.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button