Wananchi washauriwa kutumia bidhaa za ndani

KAMPUNI ya Jambo group (JAMUKAYA) iliyopo mkoani Shinyanga imejivunia katika uzalishaji wa bidhaa zake kwa zaidi ya miaka 22 na kuwashauri wananchi kuendelea kutumia bidhaa zinazotengenezwa na kampuni za wazawa ili kukuza uchumi wa nchi na mtu mmoja mmoja.

Ushauri huo umetolewa leo na Msimamizi wa Kampuni ya Jambo Group na Jambo Media, Nickson George wakati wa kuzindua chapa ya Celebratika na Jamukaya kwa wateja wa mkoa huo katika msimu wa kuelekea sikukuu ya Krismas na mwaka mpya.

George amesema wamekuja na neno Celebretika na Jamukaya au kinyumbani katika msimu wa sikukuu kwa kuhakikisha wanatoa furaha zaidi kwa wananchi wa kanda ya ziwa nakuomba waendelee kuamini zaidi bidhaa sababu zimekuwa zikitengenezwa kwa ubora.

Advertisement

“Tunataka wateja wetu wapate vitu vinavyotoka kwa watanzania wenzao na kampuni ya Jambo imekuwa ni mojawapo ya kuzalisha bidhaa za nyumbani nakuwashauri kuzitumia katika familia zao hivyo wasidharau wanapozitumia watakuwa wamekuza uchumi ndani ya nchi yao,” amesema George.

Kampuni ya Jambo Group imekuwa ikitengeneza bidhaa zake mbalimbali kwa zaidi ya miaka 22 hivyo hakuna budi ya kuwapongeza wateja kwa kuendelea na safari hii ambayo imefanya wao wajiamini kupitia bidhaa wanazozitengeneza.