Wanaofanya magendo kwenye kahawa kukiona

SERIKALI mkoani Kagera imejipanga kukabiliana na suala la magendo ya kahawa huku ikiahidi kuwachukulia hatua wale wote watakaobainika wakijihusisha na magendo hayo.

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Erasto Siima kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera,  Fatma Mwassa  akizungumza katika mkutano mkuu wa 35 wa Chama cha Ushirika KCU LTD kinachowahudumia wakulima wa kahawa wilaya za Bukoba, Muleba na Missenyi.

Sima amesema kuwa serikali ya awamu ya sita imeamua kuweka mkazo na nguvu zaidi katika kuimarisha mazao ya kimkakati hasa zao la kahawa hivyo kwa yeyote atakayejihusisha na magendo ya kahawa atachukuliwa hatua kali za kisheria .

“Magendo ya kahawa si tu yanaleta umaskini kwa Wakulima yanaikosesha pia serikali mapato na kurudisha nyuma maendeleo ya nchi, uwezi kuuza kahawa  katika nchi nyingine alafu unataka serikali ikuhudumie kwa kuweka huduma za msingi wakati wewe mwenyewe unaihujumu kwa kuuza mazao nchi nyingine tutawashughukia,”amesema Sima.

Amesema kuwa  zipo faida lukuki za  kukusanya kahawa pamoja ambazo ni kuimarisha viwanda vya ndani vinavyochakata kahawa na kuchangia ajira nyingi za vijana,  kuimarisha vyama vya ushirika , Kuongeaza takwimu za kuzalishaji katika soko la dunia.

Aidha amehimiza uthibiti ubora wa kahawa hadi kuvunwa na hatimaye kupelekwa sokoni ikiwa safi ili kupata bei nzuri sokoni kwani Kuna wimbi kubwa na wakulima wanaovuna kahawa mbichi jambo linalopoteza ubora wa Kahawa katika soko la dunia.uiba kahawa ya wakulima hivyo wakulima wanavuna kahawa mbichi jambo hilo. “Natambua Kuna changamoto za Vijana na watu wasiowatakia wakulima mema wanavamia mashamba na limeanza kupoteza ubora wa Kahawa  yetu ,naomba tuendelee kupambana na changamoto tuhakikishe ulinzi wa kahawa ili tusiharibu ubora,” amesema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi Chama Kikuu cha Ushirika cha Kagera – KCU(1990) LTD Ressy Mashulano amesema bodi hiyo inakusudia kuomba mkopo kutoka benki ya maendeleo ya kilimo(TADB) na Benki nyinginezo kiasi cha Sh bilioni 27 ambapo Sh bilioni 20 zitatumika kununulia kahawa kwa wakulima na kulipa gharama za  kuendeshaju  huku Sh bilioni 7 ikitumika katika ujenzi wa hoteli mpya ya lake.

Aidha mashulano aliwasilisha  shukrani za ushirika  kwa uongozi wa Mkoa wa Kagera chini ya Mkuu wa mkoa huo, Fatma Mwassa kwa kusimamia vyema ushirika huo, wakuu wa wilaya ikiwemo Missenyi, Muleba, Bukoba pamoja na viongozi wa halmashauri wakiwemo wenyeviti, wakurugenzi kwa kuwaunga mkono katika shughuli za uzalishaji wa kahawa.

Respicius Jonh ambaye ni mjumbe wa mkutano mkuu KCU ametumia fursa hiyo kukishauri chama hicho kuona namna ya kushughulikiwa mizani ya kidigitali kutokana na kubainika kuleta hasara kwenye vyama vya msingi  ambapo wakati mwingine inaongeza kilo wakati mwingine kupunguza kilo.

Mkutano huo uliwakusanya wanachama kutoka Wilaya za Misenyi, Muleba, Wilaya ya Bukoba  ili kujadili kwa pamoja changamoto na mafanikio  ya zao la kahawa mkoani Kagera ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati ya kufungua msimu mpya wa kahawa utakaoanza Mei mwaka huu.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button