Wanasheria: Rais hajavunja Katiba kuongeza muda Jaji Mkuu

BAADHI ya wanasheria wamesema uamuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan kuongeza muda wa kukaa ofisini kwa Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Hamis Juma sio kuvunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wakizungumza wakati wa majadiliano maalumu yaliyoongozwa na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) jijini Dar es Salaam wanasheria hao wamesema hakuna sehemu katika Katiba inaonesha Jaji Mkuu akifikisha umri wa kustaafu asiongezewe muda.

Prof. Ibrahim Juma amefikisha miaka 65. Wakili Alex Mgongolwa na Wakili Francis Stolla hawakubaliani na maneno kuwa uamuzi wa Rais ni kinyume cha Katiba.

“Hakuna maneno kwenye Katiba yanayosema Jaji Mkuu akifikisha umri wa miaka 65 hawezi kuongezewa muda. Kumbakiza Jaji Mkuu kwenye kiti chake, au kumfanya aendelee kukaa kwenye ofisi yake siyo kinyume na Katiba, bali ni kwa mujibu wa Katiba hiyo hiyo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” amesema Wakili Msomi Stolla.

Kauli ya Mawakili hao inakuja siku chache baada ya maneno kusambaa kwenye mtandao wa kijamii kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amevinja Katiba kwa kumwongezea Jaji Mkuu wa Tanzania muda wa kukaa ofisini baada ya kufikisha umri wa miaka 65.

Wamesema kuwa hakuna Ibara, wala maneno yoyote katika Katiba yanayosema umri wa kustaafu wa Jaji Mkuu, ukienda kusoma kwenye Ibara inayohusu umri wa kustaafu wa Jaji wa Mahakama ya Rufani, yanayohusiana na kumbakisha Jaji wa Mahakama ya Rufani hayatatumika kwa Jaji Mkuu.

“Vinginevyo, watunga Katiba wangekusudia hivyo wangesema umri wa kustaafu Jaji Mkuu ni sawa sawa na ule a Jaji wa Mahakama ya Rufani, isipokuwa kuendelea kukaa kwenye ofisi haitamhusu Jaji Mkuu,” Wakili Msomi Stolla amesema.

Mawakili hao wamebaisha kuwa kuwa Ibara ya 118 (2) haitamki umri wa kustaafu wa Jaji Mkuu wala Jaji wa Mahakama ya Rufani, bali umri wa kustaafu kwa viongozi hao unapatikaana kwenye Ibara ya 120 ya Katiba.

“Ili uweze kujua umri wa kustaafu wa Jaji wa Mahakama ya Rufani lazima uende kwenye Ibara ya 120 (1) ambayo imetamka miaka 65, hivyo umri wa Jaji Mkuu kustaafu ni miaka 65 kama ilivyo kwa Majaji wengine wa Mahakama ya Rufani,” amedokeza Wakili Msomi Mgongolwa.

Hata hivyo, Mawakili hao wamesema Ibara hiyo ya 120 ya Katiba inapaswa kusomwa sambamba na Ibara zake ndogo.

Rais Samia Suluhu HassanWamesema ukisoma Ibara ndogo ya (2) inasema Jaji wa Mahakama ya Rufani akishafikisha umri wa miaka 65, Rais anaweza kuelekeza asitoke kwenye ofisi ya Jaji wa Rufani, huku Ibara ndogo ya (3) inasema kuwa kama kwa manufaa ya umma, Rais ataona Jaji wa Mahakama ya Rufani anapaswa kuendelea, ataelekeza hivyo na Jaji mhusika atakubali kwa maandishi.

“Hivyo umri wa Jaji Mkuu wa kustaafu utaupata kwenye Ibara ya 120 kwa kusoma ibara zake zote ndogo. Hivyo, kuna uwezekano kwa Jaji Mkuu kuwa ofisini akiwa zaidi ya umri wa miaka 65. Hakuna katazo hilo kwenye Katiba,” Wakili Msomi Stolla amesisitiza.

Mawakili hao wamesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiona Jaji Mkuu, ambaye umri wake wa kustaafu ni sawa sawa na ule wa Jaji wa Mahakama ya Rufani, asiondoke ofisini kwa mujibu wa Ibara ya 120 (2) au aendelee kuwepo kwa manufaa ya umma kwa mujibu wa Ibara ndogo (3), anaweza kufanya hivyo.

Wametoa mfano wa mwaka 2005 ambapo Rais wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Hayati Benjamin William Mkapa alimwongezea aliyekuwa Jaji Mkuu wa Tanzania wa kipindi hicho, Mhe. Barnabas Samatta, kubaki kwenye wadhifa huo kwa kipindi cha miaka miwili.

Kumekuwepo na hoja nyingine kuhusu Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa kutotoa ushauri kwa Rais kuhusiana na suala hilo. Hata hivyo, Mawakili hao wamesema kwa mujibu wa Ibara ya 37 ya Katiba, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania halazimiki kukubaliana na ushauri wa mtu yeyote, akiwemo Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Lori L. Kent
Lori L. Kent
2 months ago

I am making easily every month $ 22000 to $ 28000 just by doing simple work from home. This job is online and very easy to do part-time or Full-time even no special experience required for this task. h96 Anyone can now participate in this job and start earning just like me by just click this link….. http://www.pay.hiring9.com

Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x