Wanawake 1200 wanufaika elimu ya malaria

Wanawake 1200 wanufaika elimu ya malaria

WANAWAKE wanaonyonyesha na wajawazito zaidi ya 1200, wamenufaika na elimu ya maambukizi ya ugonjwa wa malaria pamoja na Uviko-19, iliyotolewa na taasisi inayojihusisha na masuala ya afya kwa jamii ya Doris Mollel Foundation.

Mbali na elimu hiyo, kundi hilo kutoka mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Kagera imehamasishwa na kushiriki katika zoezi la chanjo dhidi ya Uviko-19 kutokana na elimu hiyo kwa nyakati tofauti na taasisi hiyo.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa  Taasisi hiyo, Doris Mollel, wakati akitoa taarifa yake kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Global Fund, Peter Sands, katika kikao kilichofanyika Dar es Salaam na kuongeza kuwa elimu hiyo ilianza kutolewa Desemba mwaka jana.

Advertisement

Katika kikao hicho, Mkurugenzi huyo amesema wakati wa utekelezaji wa jambo hilo, chini ya mradi wa Global Fund nchini, Doris Mollel Foundation iliwagusa makundi ya umri wote ya wanawake.