Wanawake 5 wafanyiwa upasuaji kupitia matundu madogo

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili kwa kushirikiana na wataalamu wa Alsalam Internatinal Hospital ya nchini Misri, imefanya kambi ya upasuaji wa kupitia matundu madogo (Laparoscopy surgery) kwa muda wa siku mbili, ambapo wanawake watano wamenufaika na matibabu hayo.

Akizungumza wakati wa kufunga kambi hiyo leo jijini Dar es Salaam, daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake na upasuaji wa matundu madogo wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dk Vincent Tarimo, amesema waliofanyiwa upasuaji huo wengi walikuwa na changamoto ya uvimbe kwenye kizazi.

“Upasuaji wa matundu madogo hufanyika kwa kutoboa sehemu ndogo ya mwili kwa kuingiza vifaa maalumu, ambapo una faida nyingi kwa kuwa mgonjwa hapati majeraha makubwa na uvujaji wa damu hivyo kupona haraka, ili kuendelea na shughuli zake baada ya muda mfupi,” amesema Dk Tarimo.

 

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Kim
Kim
3 months ago

Last month i managed to pull my first five figure paycheck ever!!! I’ve been working for this company online for 2 years now and i never been happier… They are paying me $95/per hour and the best thing is cause i am not that tech-savy, they only asked for basic understanding of internet and basic typing skill… It’s been an amazing experience working with them and i wanted to share this with you, because they are looking for new people to join their team now and i highly recommend to everyone to apply… 

Visit following page for more information………..>>>  http://www.Richcash1.com

Last edited 3 months ago by Kim
Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x