DAR ES SALAAM; Wanawake wametakiwa kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji utakaofanyika nchi nzima Novemba 27, mwaka huu.
Akizungumza kwenya mjadala ulioandaliwa na Daily News Digital, kwenye Jukwaa la Space la mtandao wa X wa HabariLeo, kuhusu ushiriki wa mwanamke katika uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji mwaka 2024,Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (Tamisemi), Ntenghenjwa Hoseah, amesema wanawake wana fursa za kutosha kwenye uchaguzi huo katika makundi mbalimbali.
Amesema upande wa ujumbe wanawake wanaweza kuwania katika kundi la wote bila kujali jinsia, lakini pia wanaweza kuwania katika kundi maalumu la wanawake watupu na wanaweza pia kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa kijiji au mtaa.
Soma pia: Wapeni nafasi wanawake mitaa, vijiji
Naye , mwanahabari Beatrice Bandawe, amesema anaamini wanawake wanaweza kufanya vizuri, muhimu ni hamasa iongezwe kwao wajitokeze kuwania uongozi.
Amesema anaamini wanawake wanaweza kufanya mambo makubwa, kinachotakiwa ni vyama kuwapa nafasi na kuwamini.