DAR ES SALAAM; Vyama vya siasa vimetakiwa kuwapa nafasi zaidi wanawake kuwania uongozi wa serikali za mitaa na vijiji, kwani kuna faida kubwa kwao.
Akizungumza kwenya mjadala ulioandaliwa na Daily News Digital, kwenye Jukwaa la Space la mtandao wa X wa HabariLeo, Kadete Mihayo, ambaye ni Mwanasheria Ofisi ya Rais (Tamisemi), amesema wanawake wanaweza kuwania uongozi kwenye makundi tofauti.
Soma pia: TAMWA wapongezwa wanawake kuwania uongozi
Amesema mwanamke anaweza kuwania ujumbe katika kundi la wanawake, lakini anaweza kuwania katika kundi la jinsia zote na akawania pia uenyekiti wa kijiji au mtaa, tofauti na ilivyo kwa wanaume ambao kwa ujumbe wanawania kwa eneo moja la wote tu na sehemu ya uenyekiti wa kijiji au mtaa.