Wanawake NM-AIST waanza kunogesha siku ya wanawake

WANAWAKE wa  Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) wameungana  na wanawake wengine jijini Arusha kushiriki mbio za Wanawake ‘Women’s Fun Run2025’.

Mbio hizo zimehusisha urefu wa kilomita 10 na kilomita 5,  ikiwa ni shamrashamra kuelekea Siku ya Wanawake Duniani itakayofanyika kitaifa jijini hapo Machi 8, 2025.

Mbali na mbio hizo kumekuwa na michezo mbalimbali ya jadi ikiwemo mdako, bao, kukimbia na maguni, kuvuta kamba pamoja na rede ambapo NM-AIST imeibuka mshindi wa pili, ambapo mshindi wa kwanza ni Jeshi la Zimamoto na wa tatu TEMDO.

Hata hivyo wanawake hao walipongeza uwepo wa michezo ya zamani katika kuimarisha afya ikiwemo mchezo wa mdako unaondoa makunyanzi usoni na kuleta nuru ya uso.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button