Wanawake vyombo vya ulinzi Manyara watakiwa kujiweka sawa kiuchumi

MANYARA: WANAWAKE wa vyombo vya ulinzi na usalama Mkoa wa Manyara wamejengewa uwezo katika kusimamia vizuri malezi na makuzi ya familia zao na kujiimarisha kiuchumi.
Mrakibu Mwandamizi wa Polisi ambaye ni Mkuu wa Polisi Wilaya ya Babati, Ernesta Mwambinga amesema lengo ni kujengea uwezo askari wa kike mkoani humo katika nyanja za kiuchumi, kiafya.

Amesema hayo kwenye mafunzo ya uwezeshaji, kuongeza ufanisi, kuimarisha uongozi na kujenga uchumi kwa wanawake wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoa wa Manyara.
Amesema wajibu huo ni kutekeleza majukumu ya kazi wanapokuwa kazini na wakati wakiwa majumbani kutekeleza majukumu ya familia kama mama, mlezi na mlinzi mkuu wa familia.

”Mafunzo yamekumbusha wajibu wa kuheshimu ndoa,kutoa malezi bora kwa watoto kama walivyo imara katika utendaji wao wa kazi,” amesema Mwambinga.
”Tukiangalia dunia ilivyo sasa, sera ya nchi inatutaka kujenga uchumi kuanzia mtu mmoja mmoja na askari wanahitaji kuimarisha uchumi na kujua mipango ya utunzaji wa fedha,”amesisitiza Mwambinga.
Kwa mujibu wa Mwambinga wanawake wanapokuwa katika hali nzuri ya kifedha wataweza pia kuihudumia jamii kwa weledi na usafi.

Mrakibu mwandamizi wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Manyara ambaye ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanawake Magereza Mkoa wa Manyara, Elizabeth Morembwa amesema mafunzo hayo yatasaidia kuimarisha utoaji wa huduma za kurekebisha tabia za wafungwa ili wanapotoka gerezani waweze kuwa raia wema.
Mafunzo hayo yamefunguliwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora, Regina Ndege ambaye amewahimiza wanawake wa vyombo vya ulinzi na usalama kuchangamkia fursa za kiuchumi kama wanawake wengine ili kuongeza kipato badala ya kutegemea mishahara pekee.




thisis a fantastic article, really nice created, i enjoy reading it, i will be back to check out for latest update, keep up the good work and applause. gh.yandaz.com