Wanawake wahamasishwa kukopa na kurudisha

Wanawake wahamasishwa kukopa na kurudisha

UMOJA wa Wanawake (UWT) tawi la Sinza, Dar es Salaam wamesema ni wakati wa wanawake kuamka na kukopa ili kujishughulisha masuala ya kiuchumi.

Wametoa kauli hiyo wakati wa tamasha lao liitwalo Usiku wa Mama’s lililofanyika jana usiku, ambapo pamoja na mambo mengine walimshukuru Rais Samia Suluhu Hassna kwa serikali yake kutoa mikopo kwa wanawake.

Akizungumza na HabariLeo, Katibu wa Wanawake UWT, Sara Mwakalebela, amesema ni wakati wa wanawake kuamka na kujishughulisha kukopa na kurudisha, ili kusaidia wengine kupata mikopo.

Advertisement

“Tunamshukuru Rais Samia kwa kutupa kipaumbele wanawake kufanya maendeleo katika familia, jamii na taifa, wanawake tunaweza ni jeshi kubwa,” amesema Sara.

Amesema wapo wanawake wengi walionufaika na mikopo mbalimbali, ambapo wanajivunia mikopo hiyo.

“Mnufaika sio kukopa tu bali kufanyia kazi na kurudisha mkopo sehemu husika, ili wenzako waweze kunufaika na mkopo huo pia, ” alisema.

Alisema hawataishia kusherehekea tu, bali wataenda mbali zaidi na kusaidia kusaidia jamii.