Wanne mbaroni kwa wizi msibani, msikitini

ZANZIBAR; POLISI Mkoa wa Kusini Unguja inawashikilia watu wanne kwa tuhuma za wizi wa pikipiki katika maeneo ya mikusanyiko ya watu ikiwemo kwenye harusi, misiba na nyumba za ibada.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja,  Daniel Shillah, amewataja watuhumiwa hao ni Iddi Abdallah Kisumba (20), Rashid Abdallah Sadala (19 ) wote wakazi wa Kidimni.

Watuhumiwa wengine ni Fakih Kassim Khamis (19) mkazi wa Amani na Ahmed Amour Abdalla (24), mkazi wa Makunduchi, ambao wamekamatwa maeneo tofauti wakiwa wameiba pikipiki tatu.

Kamanda Shillah amesema pia wamekamata watu wengine watatu wakituhumiwa kujihusisha na unyang’anyi wa kutumia silaha kwa kuwavizia watembea kwa miguu na kuwatishia kwa mapanga, kisha kuwapora kwa kutumia pikipiki.

Watuhumiwa hao ni Khalid Salum Said (20) na Yassir Abdalla Shaaban (30) wote wakazi wa Fuoni na Ali Mohamed Ali ‘Shetani Kiro’ (28) mkazi wa Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja.

Habari Zifananazo

Back to top button