Wanyamapori kuwekewa uzio kudhibiti athari

DODOMA : NAIBU WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dunstan Kitandula amesema serikali itaendelea kuweka uzio katika baadhi ya maeneo ya hifadhi ya wanyamapori ili kudhibiti athari zinazotokana na wanyama kuingia maeneo ya makazi ya watu.

Akijibu swali bungeni jijini Dodoma, Naibu Waziri Kitandula amesema mpango wa serikali ni kuhakikisha ulinzi katika maeneo yote ya hifadhi unaimarishwa, ili kuzuia maafa na madhara yanayosababishwa na wanyamapori kwa wananchi wanaoishi karibu na hifadhi hizo.

“Serikali itahakikisha maisha ya Watanzania yanalindwa,” alisema Kitandula.

Amesema hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za serikali kulinda maisha na mali za wananchi dhidi ya mashambulizi ya wanyama kama tembo, simba na wengineo ambao wamekuwa wakiharibu mashamba na kusababisha vifo katika baadhi ya maeneo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button