Waogeleaji 70 wenye ulemavu kushindana Dar

WAOGELEAJI 70 wenye ulemavu wanatarajiwa kushindana Oktoba 12 katika mashindano ya pili ya kitaifa ya kuibua vipaji yakayofanyika, Upanga Dar es salaam.
Katika Mkuu wa Chama cha Kuogelea kwa watu wenye ulemavu (TPSA) Ramadhan Namkoveka ameiambia HabariLeo Online kuwa waogeleaji wenye changamoto mbalimbali ikiwemo ulemavu wa viungo, ngozi, macho na usonji wataonesha vipaji vyao.
SOMA: TPSA sasa kwenda kimataifa
“Kamati yetu ya maandalizi ya mashindano ikiongozwa na Thauriya Diria akisaidiwa na Clara Kiziga inafanya kila juhudi kuhakikisha mashindano haya yanafanyika kwa mafanikio makubwa,”amesema.
Amesema wachezaji watakaofanya vizuri watachaguliwa kwenye timu ya Taifa kwa ajili ya kupatiwa mafunzo zaidi na kuweza kushiriki mashindano kadhaa ya kimataifa.
Namkoveka amesema changamoto ni nyingi na bila ya msaada wa wadau mbalimbali wakiwemo familia ya kuogelea, makampuni na watu binafsi hawataweza kufanikiwa na kufikia malengo waliyojiwekea.
Mgeni Rasmi wa mashindano hayo anatarajiwa kuwa Rais wa Kamati ya Paralimpiki Tanzania (TPC) Provian Dandi.
Mashindano hayo yatatumika kupima afya bure kwa wananchi wote ambao watapenda kujua afya zao.



