Wapalestina 200 wameuawa mwaka huu

ZAIDI ya Wapalestina 200 na Waisraeli 30 wameuawa mwaka huu katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa na Israel kutokana na ghasia za mataifa hayo, imeripotiwa ni idadi kubwa zaidi ya vifo tangu 2005, mjumbe wa Umoja wa Mataifa Mashariki ya Kati amesema.

Tor Wennesland, mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa katika mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati, aliliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana kwamba kuongezeka kwa ghasia kunachochewa na kuongezeka kwa hali ya kukata tamaa kuhusu mustakabali wa Wapalestina na ukosefu wa maendeleo ya kufikia taifa huru.

“Wapalestina na Waisraeli wanauawa na kujeruhiwa katika ghasia za kila siku ikiwa ni pamoja na saa chache kabla ya mkutano huu shambulio lingine limemuuwa Muisraeli katika Ukingo wa Magharibi,” aliambia Baraza la Usalama, akizungumza kutoka Jerusalem.

Advertisement

Wakati Waisraeli na Wapalestina wakichukua hatua za kuleta utulivu wa hali ya sasa, Wennesland alisema hatua za upande mmoja zimeendelea kuzidisha uhasama.

Ameashiria upanuzi wa haraka wa vitongoji vya walowezi wa Israel, ubomoaji wa Israel wa nyumba za Wapalestina, operesheni za wanajeshi wa Israel katika maeneo ya Ukingo wa Magharibi yanayokaliwa kwa mabavu chini ya udhibiti wa utawala na polisi wa Palestina, na mashambulizi ya walowezi wa Israel kwenye vijiji vya Wapalestina.

Wennesland pia alitaja “shughuli za kijeshi” za Palestina, na akasema kwamba hali ya sasa inachangiwa na “udhaifu” wa hali ya kifedha ya Mamlaka ya Palestina pamoja na uhaba mkubwa wa fedha unaokabiliwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa ikiwa ni pamoja na wakala wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA.

“Ingawa ni lazima tuzingatie kwa haraka kushughulikia masuala muhimu zaidi na kupunguza hali hiyo, hatuwezi kupuuza haja ya kurejesha upeo wa kisiasa,” alisema.

“Wajumbe wa baraza walie wazi leo kwamba vurugu lazima ikome. Nawaomba viongozi wachukue hatua sasa ili kutuliza hali. Msururu huu wa vurugu hauelekei popote ila kwa umwagaji damu zaidi,” Wennesland alisema kwenye mtandao wa kijamii.

9 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *