Wapigwa msasa sheria ununuzi wa umma

WIZARA ya Fedha inaendelea kutoa mafunzo kuhusu sheria ya ununuzi wa umma katika Mkoa wa Mtwara, Lindi na Ruvuma.

Mafunzo hayo yaliyofanyika leo Septemba 6, katika Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara yatakuwa ya siku moja.

Advertisement

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria kutoka kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta binafsi (PPPc) Flora Tenga amesema lengo la mafunzo ni kuelimisha maofisa mipango na viongozi wote wanaohusiana na ununuzi ili kufahamu fursa zilizopo katika sheria hiyo na namna wanavyokwenda kuitekeleza.

Amesema sheria ya ubia kati sekta ya umma na sekta binafsi imetoa fursa mbalimbali katika miradi ya ubia ambapo kuna fursa na vivutio vingi vinavowavutia wawekezaji.

Hata hivyo amewataka wote wanaotekeleza miradi ya maendeleo, badala ya kusubiri  fedha za serikali kutekeleza miradi ya maendeleo  atumie sheria hiyo kumwalika mbia mwekezaji aweze kuleta fedha za kutekeleza miradi hiyo ya maendeleo ikiwemo miradi midogo midogo inayotekelezwa kwenye halmashauri.

Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Ununuzi wa Umma (PPRA) Kanda ya Kusini, Fenias Manasseh amesema wamelazimika kutoa mafunzo hayo kwa watumishi wa serikali kutoka sekta mbalimbali ili kuwapatia elimu hiyo ya sheria ya ununuzi wa umma ili  waweze kujua fursa na mabadiliko yaliyopo kwenye sheria hiyo ili waweze kufaidika nazo.

SOMA: Wizara ya Fedha yaliomba Bunge Sh tril.18.17

“Hapa waliyo wengi ni taasisi nunuzi wanaofanya kazi ya michakato ya ununuzi sasa kama hawaelewi mabadiliko yaliyojitokeza kwenye sheria ya ununuzi wa umma wataendelea kuwa na mambo ya kizamani kwahiyo wahusika wanashindwa kufaidi hizi fursa nyingi mbalimbali za maendeleo”amesema Manasseh.

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara, Abdillah Mfinanga amesema wizara hiyo inaendesha mikutano kwa watendaji wa serikali waliyopo katika ngazi za mikoa, halmashauri, majiji, miji na wilaya kufuatia kuwepo kwa changamoto mbalimbali zinazohusu utekelezaji wa sheria hiyo.

SOMA: Wizara ya Fedha Walindeni watumiaji wa huduma za fedha

Aidha mada zilizowasilishwa katika mafunzo hayo ikiwa ni pomoja na utekelezaji wa sheria ya ununuzi wa umma lenye lengo la kuwafahamisha watanzania juu ya fursa mbalimbali zinazopatikana katika sheria hiyo.