Wasaidia yatima, wajane Temeke

TAASISI ya kiislamu ya Muslim Word League, imepokea msaada wa maboksi 510 ya vyakula  kutoka serekali ya Saudia Arabia kwa ajili ya yatima na wajane katika Manispaa ya Temeke, ikiwa ni sehemu ya kusaidia kumudu mahitaji yao muhimu katika maisha ya kila siku.

Msaa huo umetolewa leo Agosti 5, 2023  jijini Dar es Salaam, ambapo msaada uliotolewa ni mchele10, maharage, ngano ,sukari  na mafuta ya kula.

Baadhi ya wanufaika na msaada huo wameshukuru kwa hatua hiyo, kwani imewafuta machozi na kupunguza changamoto zinazowakabili,  huku Meya Manispaa ya Temeke Abdallah Mtinika akiomba mashirika kujitokeza zaidi.

Mkurugenzi wa taasisi hiyo Sheikh Hassan Katungunya, ameshukuru na kupongeza waislamu wote walioko Saudia Arabia kwa walichotoa kwa Watanzania.

 

Naye mwakilishi wa Balozi wa Saudia Arabia, Dk Fahad Ahabby amesema msaada huo utakuwa endelevu ili kuhakikisha yatima na wajane wanapata mahitaji yao muhimu.

Habari Zifananazo

Back to top button