Foundation for Civil Society (FCS) na Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za za Usafiri Ardhini (LATRA CCC) wamesainiana Mkataba wa Makubaliano (MoU) wa miaka mitatu ili kuimarisha ulinzi wa watumiaji wa usafiri.
Ulinzi wa walaji na haki zao ndani ya sekta ya usafiri ili kuwe na huduma bora kwa Wasafirishaji na wasafiri kwa kuwa ni huduma inayotumika kila siku.
Akizingumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Justice Rutenge amesema kuungana kw FCS na LATRA CCC wanakusudia kuunda mazingira bora ya walaji katika sekta ya usafiri wa ardhi, kukuza taratibu bora za kibiashara na kuhamasisha ukuaji wa biashara.
Amesema ushirikiano huo unalenga kuwakilisha maslahi ya walaji wanaotumia usafiri wa ardhi ulio na udhibiti kwa ajili ya bidhaa na huduma katika nchini ambapo itahakikisha wasafiri na wasafirishaji kwa njia ya ardhini wanapata huduma bora zenye kukidhi matakwa ya kitaifa na kimataifa.
Pia Ushirikiano huo wa kimkakati utahusisha kubuni na kutekeleza mipango inayokuza haki za walaji na kulinda bidhaa na huduma za usafiri wa ardhi zinazodhibitiwa.
Wakati wa hafla ya kusaini Mkataba wa Makubaliano, Mkurugenzi Mtendaji wa FCS alisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika kuimarisha uwezo wa raia na nguvu za ulinzi wa walaji.
Alisema, “Kwa miongo miwili iliyopita, FCS imeweka mtazamo wa kuzingatia raia, ikilenga kukuza uwezo wa raia. Ahadi yetu ya kulinda walaji inatokana na dhana hii.”
Rutenge alifafanua kuhusu haki muhimu ambazo walaji wanazo, ikiwa ni pamoja na haki ya kupata malipo ya haki kwa madai, elimu kuhusu usafiri wa ardhini, wa bidhaa na huduma, na uhakikisho wa ubora.
“Katika kushirikiana na LATRA CCC, wadau muhimu katika kukuza ulinzi wa walaji katika sekta ya usafiri wa ardhi, FCS itatumia utaalamu wake katika kujenga uwezo kusaidia LATRA CCC katika kutafuta rasilimali muhimu za kutekeleza mipango inayolenga kulinda haki za walaji nchini Tanzania,” alieleza.