Wasanii wajitosa kutangaza utalii

WATANGAZAJI maarufu nchini Lilian Mwasha, Maimartha Jesse na Mc Pilipili, wameamua kumuunga mkono Rais Samia Suluhu kuhamaisha utalii wa ndani kwa kutembelea hifadhi mbalimbali za Taifa kupitia kampeni ya Temboka na Tanapa.

Mbali na watangazaji hao pia waimbaji Flora Mbasha, Mariam Kilyenyi, Grace Sangija, wameungana kwenye uhamasishaji huo wakishirikiana na Shirika la Hifadhi la Taifa (TANAPA).

“Tumeamua kumuunga mkono Rais Samia katika kutangaza utalii wa ndani na sasa tumeanza kutembelea mbuga ya Tarangile,” amesema Mariam Kilyenyi

Amesema jamii inapaswa kujijengea mazoea ya kufanya utalii kwenye mbuga za wanyama nchini ili kutangaza vivutio vilivyopo.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x