DAR ES SALAAM: WASANII wametakiwa kutunza vipaji vyao kwa kuwa ndio vinavyowapatia fursa ya vipato.
Kaimu Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu, Dk Gervas Kasiga amesema hayo leo wakati wa uzinduzi wa Washirika wa Tamasha na Tuzo za Filamu Tanzania 2025.
Dk Kasiga amesema tamasha hilo lenye kauli mbiu ya ‘Filamu ni biashara’ amesisitiza kuwa vipaji ndio sehemu kubwa ya kutoa ajira
Amesema tamasha hilo linaratibiwa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bodi ya Filamu Tanzania pamoja na Studio 19 Limited.
“Linapozinduliwa tamasha la nne ubora unaongezeka, linaambatana na upatikanaji wa filamu, mchujo wa filamu kisha mfululizo wa mafunzo kwa wadau na kongamano kwa wadau wa filamu.
“Wizara inaelekeza kuhakikisha sekta binafsi inashirikishwa nio maana studio 19 imeshirikishwa mwaka huu 2024,” amesema.
Amesema lengo la tamasha hilo ni kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kuanzisha na kuratibu program za kufufua, kukuza na kuendeleza vipaji vya wanafila.
Amesema Rais Samia ameonesha ana mapenzi na tasnia ya filamu kwa kuwa hata yeye alishiriki katika kutengeneza filamu.
Naye Mkurugenzi wa Filamu 19, Sama Jahanpour amesema nguvu iliyokuwak wenye sanaa ya filamu ni nyenzo muhimu katika kueneza sanaa za masimulizi.
Pia amesema picha jongefu ina nguvu ya kufikia watu wengi, vile vile ina nguvu kubwa ya kuhamasisha watu.
Kwa upande wake Mkurugenzi, Studio 19 Limited, Brian Paul amesema uzinduzi huo utawaweka wadau kutoka sekta mbalimbali za ubunifu pamoja ili kuorodhesha mustakabali wa tasnia hiyo.
“Tamasha la Filamu na Tuzo za Tanzania 2025 ni mpango kabambe unaolenga kuiweka Tanzania kama kitovu cha ubunifu wa kimataifa, kwa kutumia uwezo wa filamu kukuza utamaduni, kusukuma ukuaji wa tasnia na uvumbuzi wa nishati.
‘Uzinduzi huu ni hatua muhimu katika safari hii, iliyoundwa ili kukuza mazungumzo, kuhamasisha ushirikiano, na kuoanisha malengo ya pamoja ya tamasha,” amesema.
Amefafanua kuwa tamasha hilo dhamira yake ni kutumia uwezo wa kusimulia hadithi kwa ajili ya mabadiliko ya kijamii na kiuchumi.
Amesema tamasha hilo litafichua vipaji ambavyo havijatumiwa katika tasnia ya ubunifu, kuunganisha
Washika dau mbalimbali na kukuza uwezo wa sekta hiyo kuleta mabadiliko yenye matokeo.