Wasanii wasisitizwa vyanzo vya mapato endelevu

DAR ES SALAAM: WASANII wa filamu nchini wametakiwa kujikita kutafuta vyanzo endelevu vya mapato ili kujihakikishia maisha bora ya sasa na ya baadaye, huku wakihimizwa kuongeza ushindani wao katika soko la kimataifa.

Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam na Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Mahudhui na Utangazaji wa Azam Media, Yahya Mohamed Kimaro, wakati wa uzinduzi wa filamu nne mpya zitakazoonyeshwa kupitia Azam Max.

Filamu hizo ni The Green Tanzanite, My Son, Couple Goal, na Jenina, ambazo zitaanza kuonyeshwa rasmi kupitia jukwaa hilo la kidijitali.

Akizungumza katika hafla hiyo, Kimaro alisema Azam Media imelenga kutoa huduma jumuishi na rahisi kufikika kwa watazamaji wa ndani na nje ya nchi.

“Tumetoka kwenye kipindi cha kukimbizana na kukamata CD na DVD, sasa tunaanza kufurahia matunda ya kazi zetu kwa kushirikiana kimataifa zaidi,” amesema Kimaro.

Kwa upande wake, Mkuu wa Chaneli ya Sinema Zetu, Sofia Mgaza, aliwataka wasanii kurejesha heshima ya tasnia ya filamu kama ilivyokuwa miaka ya nyuma, huku wakizingatia maadili na ubora wa kazi zao wanapoingia katika soko la kimataifa.

Naye Ignasi Mkindi, kiongozi wa filamu ya The Green Tanzanite, alisema hapo awali walikumbana na changamoto kubwa ya uharamia wa kazi zao kupitia CD na DVD, lakini sasa wanafurahia mafanikio ya juhudi zao.

Isalito Mwakalindile aliwahimiza wasanii kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kushindana kimataifa badala ya kujikita katika soko la ndani pekee.

Kwa niaba ya waongozaji wa maudhui, Adam wa Noma aliwasihi wasanii kuendelea kufanya kazi kwa ubunifu na kujitangaza ili kukuza soko la filamu nchini.

Aidha, mwongozaji wa Couple Goal, Manka, alisema ana shauku kubwa na kazi yake, na ameahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuimarisha nafasi yake katika tasnia ya filamu na kuvutia soko zaidi.

Ameongeza kuwa filamu hizo zitapatikana kwa gharama nafuu kulingana na maeneo tofauti, ambapo nchini Tanzania watazamaji watalipa nafuu, Kenya , Uganda za Uganda, na kwa watazamaji wa kimataifa gharama ni dollar

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button