Washauri ulinzi dhidi ya watoto kuepuka ukatili

WADAU wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) mkoani Pwani wameshauri jamii kuwalinda watoto ili kuepukana na vitendo vya ukatili.

Hayo yalisemwa Mjini Kibaha na Mkurugenzi wa Anjita Child Development Foundation Janeth Malela wakati wa kikao cha maandalizi ya uzinduzi wa Programu hiyo kwa Mkoa wa Pwani.

Malela alisema kuwa programu hiyo itasaidia kuimarisha ukuaji na maendeleo ya mtoto kikamilifu kimwili, kiakili, kukuza lugha, mawasiliano kijamii na kihisia.

Advertisement

“Programu inalenga kuimarisha utoaji huduma bora za afya, lishe, malezi yenye mwitikio, ujifunzaji wa awali na ulinzi na usalama kwa watoto wa miaka 0 hadi 8 na kuimarisha ushirikiano wa wadau wa sekta mbalimbali katika huduma za MMMAM,”alisema Malela.

Aidha alisema kuwa lengo kuu ni kusaidia watoto kwenye masuala ya malezi,makuzi,ujifunzaji,ulinzi wa mtoto,afya ili wakue katika mazingira mazuri na kukua kutokana na sheria zilizopo.

Kwa upande wake ofisa maendeleo ya jamii mkoa wa Pwani Rachel Chuwa alisema kuwa moja ya changamoto wanazozipata watoto ni baadhi ya wazazi na walezi kutowahudumia watoto wao kwa wakati kutokana na kutafuta mahitaji ya nyumbani.

Chuwa alisema kuwa malezi na makuzi wazazi wanapaswa wawahudumie lakini kwa sasa wanalelewa na televisheni na mitandao na suala la lishe shuleni baadhi wanatoa chakuka lakini waengine hawatoi hivyo mpango huo utasaidia kuondoa changamoto zolizopo ili wapate huduma stahiki.

Naye mkurugenzi wa shirika la maendeleo kwa vijana (YPC) Israel Ilunde alisema kuwa mpango huo ni muhimu sana kwani vijana wanakumbana na changamoto za kimaadili kutokana na kutopata malezi bora kutokana na hali ya kimaisha.

Ilunde alisema kuwa mpango huo utasaidia sana katika kuwalea watoto na kuondoa vitendo viovu kutokana na malezi watakayoyapata hivyo rasilimali zitengwe ili kuwalea watoto katika misingi mizuri ya kimaadili.

Mikoa 10 ambayo imeshazindua programu hiyo ni Tabora, Arusha, Morogoro, Rukwa, Manyara, Mbeya, Dodoma, Dar es Salaam, Kagera na Lindi.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *