Washington, Beijing za ahidi kushirikiana kuboresha uhusiano

RAIS wa Marekani, Joe Biden na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Xi Jinping wameahidiana kushirikiana kutatua changamoto zinazokumba mataifa mbalimbali ulimwenguni pamoja na kuboresha uhusiano wao uliodorora katika miaka ya hivi karibuni.

Wawili hao wamekutana kwenye mkutano wa nchi 20 zilizoendelea kiuchumi G20 huko Bali Indonesia.

Katika mkutano wa kwanza uliofanyika jana na kudumu kwa saa tatu, miongoni mwa ajenda zilikuwa ni masuala ya kibiashara kutoka nchini Taiwan na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Kufuatia mazungumzo hayo, Biden aliwaambia waandishi wa habari kuwa anaamini “hakuna haja ya kuwa na vita baridi mpya”, huku ofisi zao zikisema viongozi hao wawili walisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Beijing na Washington ili kukabiliana na masuala ya kimataifa.

“Biden alisisitiza kwamba Marekani na China lazima zishirikiane kushughulikia changamoto za kimataifa – kama vile mabadiliko ya hali ya hewa, utulivu wa uchumi wa kimataifa ikiwa ni pamoja na msamaha wa madeni, usalama wa afya, na usalama wa chakula duniani – kwa sababu ndivyo jumuiya ya kimataifa inatarajia,” ilisema taarifa ya Ikulu ya White House.

Shirika rasmi la habari la China, Xinhua, pia limemnukuu Xi akisema kwamba “pande hizo mbili zinapaswa kufanya kazi na nchi zote kuleta matumaini zaidi kwa amani ya dunia, imani zaidi katika utulivu wa dunia, na msukumo mkubwa wa maendeleo ya pamoja”. alisema Xi.

Mkutano huo unafuatia kuongezeka kwa mvutano kati ya nchi hizo mbili baada ya mbunge wa ngazi ya juu wa Marekani Nancy Pelosi kuzuru Taiwan mapema mwaka huu na Biden aliahidi kutetea kisiwa kinachojitawala – ambacho Beijing inadai kuwa chake – ikiwa China itaivamia.

Kuhusu Taiwan, Biden alieleza kwa kina kwamba sera yetu moja ya China haijabadilika, Marekani inapinga mabadiliko yoyote ya upande mmoja kwa hali iliyopo kwa pande zote mbili, na dunia ina nia ya kudumisha amani na utulivu.

Chini ya sera ya China Moja, Marekani inaitambua Jamhuri ya Watu wa China (PRC) mjini Beijing dhidi ya Jamhuri ya Uchina (ROC) iliyoko Taipei kama serikali pekee na ya kisheria ya Uchina. Lakini Washington haichukui msimamo wowote juu ya uhuru wa Taiwan, ikisisitiza kwamba mustakabali wake unapaswa kuamuliwa kwa njia za amani.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x