Wadau wekezeni elimu za awali

MAREKANI : MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora  Mama Mariam Mwinyi, ameshiriki mkutano pamoja na Wake wa Marais wa nchi nyengine za Afrika wanachama wa Taasisi ya OAFLAD iliyoandaliwa na taasisi hiyo kwa kushirikiana na Taasisi ya Theirworld jijini New York, Nchini Marekani.

Mama Mariam amepata fursa ya kutoa uzoefu wa Zanzibar kwenye eneo la elimu ya awali ya makuzi ya mtoto (ECD), kwamba Serikali ya Mapunduzi ya Zanzibar imefanya juhudi za kutekeleza tamko la kisera iliyobainisha wazi kuwa kila mtoto anaefikia miaka 4 ana haki ya msingi kupata elimu ya awali.

Amesema  hivi sasa  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ianendelea kufanya mapitio ya mtaala kutoka mtaala wa nadharia hadi kua mtaala wenye kujenga uwezo wa kiushindani katika elimu na kuanzisha program ya mlo mmoja kwa skuli za awali za Serikali pamoja na kufanya uchunguzi wa afya za watoto.

Kwa upande wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora, katika kuunga mkono juhudi za Serikali imetekeleza program ya Lishe kwa kufufua Wiki ya Afya na Lishe inayohamasisha kuzingatia lishe bora pamoja na kuzingatiaj uchunguzi wa kiafya katika hatua za mapema na matibabu kwa watoto zaidi ya 10,000.

Kwa upande mwengine ZMBF inatekeleza program ya Tumaini inayozingatia kutoa elimu kwa mtoto wa kike balehe zaidi ya 4,700 ya hedhi salama, lishe na afya ya akili pamoja na taula za kufua.

SOMA :Rais Dkt Mwinyi awasili Jakarta

 

Habari Zifananazo

Back to top button