Washiriki NDC wajifunza usalama wa chakula

WASHIRIKI wa kozi ya 13 kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) Tanzania wametembelea katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha TARI Naliendele mkoani Mtwara ili kujifunza mambo mbalimbali kiwemo usalama wa chakula.

Akizungumza wakati walipotembelea kutuo hicho cha  TARI Naliendele, Mkurugenzi wa Mafunzo kutoka chuo hicho, Dk Oswald Masebo amesema lengo la kutembelea kituo hicho ni kujifunza mambo ya msingi ya usalama wa chakula.

Aidha mkurugenzi huyo wa mafunzo amezungumza kwa niaba ya Mkufunzi Mwandamizi Elekezi Jeshi la Anga  kutoka chuo hicho cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Brigedia Jenerali Erick Mhoro.

‘’Suala la usalama wa chakula ni muhimu sana kwa ajili ya usalama wa taifa na tumeona namna ambavyo kiuto hiki cha utafiti wanafanya kazi bora sana katika kutafiti mbegu bora kwa ajili ya kuimarisha kilimo cha korosho, karanga, ufuta na mazao mengine,’’amesema Masebo.

Aidha, kazi hiyo inayofanyika ni mzuri katika kuchangia usalama wa taifa na kusaidia shughuli hizo za ufafiti kwani bila utafiti hawawezi kuwa na kilimo kilicho bora na chenye tija kwa wakulima pia utafiti unachoche kuwepo kwa uzalishaji mkubwa katika mazao ikiwemo zao la korosho.

Mazao yanayofanyiwa utafiti ikiwemo korosho na kuuzwa nje ya nchi taifa linakuwa na uhakika wa kupata fedha za kigezi ambazo serikali inazitumia kuboresha maisha ya watanzania, kuchochea ujenzi wa miundombinu ya kimkakati, kuimarisha uslama na ulinzi wa taifa na kutoa huduma za jamii.

Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Ismail Omari amesema suala la ulinzi kwa mapana yake siyo tu kulinda mipaka bali ni pamoja na usalama wa mtu mmoja mmoja ikiwemo kiafya na kichakula.

Kaimu Mkurugenzi wa kituo hicho cha TARI Naliendele na Mratibu wa Uhaulishaji wa Teknolojia na Mahusiano, Bakari Kidunda amesema kazi ya kituo hicho ni kufanya utafiti wa mazao mbalimbali ikiwemo korosho, ufuta, karanga, mboga mboga, matunda na mengine.

‘’Tunafanya utafiti kwa ajili ya kutatua changamoto za wakulima na kuhakikisha kuwa mkulima anapata teknolojia sahihi ili kuongeza uzalishaji wenye tija na kuongeza mapato ya taifa kwa ujumla’’amesema Kidunda.

Habari Zifananazo

Back to top button