‘Wasichana pazeni sauti mtimize malengo yenu’

DAR ES SALAAM: Shirika la Plan International Tanzania limetoa wito kwa wasichana nchini kote kujitokeza na kupaza sauti zao, ili kuweka wazi changamoto zinazowakabili katika kutimiza malengo yao ikiwemo hatamu za uongozi.

Hayo yamesemwa leo, jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Shirika la Plan International Tanzania, Jane Sembuche, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya taasisi hiyo kuelekea maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani.

Sembuche amesema kuelekea maadhimisho ya siku hiyo, shirika hilo limekuja na kampeni mbili ambazo ni Msichana Kushika Hatamu na kampeni ya Sikia Sauti Zetu, inayolenga kutoa fursa kwa wasichana kupaza sauti zao kwa mamlaka husika.

Advertisement

Aidha, amesema maadhimisho hayo yanatarajiwa kuhudhuriwa na mamia ya wasichana kutoka nchi zaidi ya 60 ambazo shirika hilo linafanya kazi.

Isome: Samia Scholarship yaleta mwamko sayansi kwa wasichana

Pia amesema maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike yanalenga kutoa elimu juu ya upatakinaji wa haki na uwezeshwaji wa wasichana duniani kote.

Pia ametoa wito kwa serikali kutatua changamoto mbalimbali zinazowakwamisha wasichana kutimiza malengo yao, ikiwemo sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kifungu cha 13 na 17, akisema kuwa kifungo hicho kinachagiza uwepo wa ndoa za utotoni.