Wasichana waliangukia Bunge mabadiliko sheria ya ndoa

WATOTO wa kike wameshirikiana na wadau mbalimbali kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Kike Duniani kwa kuliomba Bunge la Tanzania kuharakisha mabadiliko ya sheria ya ndoa ili kuzuia watoto chini ya miaka 18 kuolewa.

Kwa kupitia risala yao iliyosomwa na Genevieve Zawadi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Kichangani mjini Iringa, watoto hao wamesema wanatamani kuona ndoto zao za maisha zikitimia.

“Kama sheria zinazuia mtoto chini ya umri wa miaka 18 kupata leseni ya udereva na kufanyishwa kazi ngumu inakuwaje mtoto huyo huyo azae au kufunga ndoa akiwa chini ya umri huo kana kwamba kazi hiyo ni ndogo,” alisema.

Akipaza sauti ya watoto wa kike Zawadi alisema hii ni zamu ya bunge kubadilisha kifungu cha 13 na 17 cha sheria ya ndoa ya mwaka 1971 vinavyoruhusu mtoto wa kike kuolewa akiwa na miaka 14 kwa idhini ya mahakama na miaka 15 kwa idhini ya wazazi.

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Nancy Nyalusi amesema ni kweli sheria ya ndoa inaweza kufanyiwa marekebisho ili kumlinda mtoto kwa kuzingatia maslahi na haki zake.

Nyalusi alisema mazingira ya baadhi ya watoto hususani wa kike yanawapitisha katika changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na unyanyasaji hasa wa kingono, malezi hafifu, umasikini na udumavu.

Mwakilishi wa Shirika la World Vision Tanzania, Vicent Kasuga alisema shirika lao linafanya kazi katika mikoa 16 ikiwemo Iringa likilenga kuboresha maisha ya watoto hasa wa kike na jamii kwa ujumla kupitia miradi mbalimbali.

“Kwasasa tunatekeleza mpango mkakati wa miaka mitano 2021-2025 unaolenga kuwafikia watoto milioni 14 ambao kati yao watoto milioni 3.2 ni wale wanaoishi katika mazingira magumu,” alisema.

Kasuga alisea katika kipindi cha miaka hiyo mitano wataendelea kutekeleza kampeni yao ya Kupinga Ndoa na Mimba za Utotoni kupitia program ya ulinzi na ustawi wa mtoto.

Kwa upande wake Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Tanzania,  Mary Nzuki alizungumzia historia ya dawati hilo akisema lilianzishwa mwaka 2008 kwa ajili ya kushughuliakia masuala ya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya watoto.

“Tuna ofisi 420 za dawati zilizotapakaa nchi nzima zenye askari waliopata mafunzo kwa ajili ya kushughulikia masuala yote yanayohusu ukatili na unyanyasaji dhidi ya watoto,” alisema.

Akitoa takwimu za kitaifa za ukatili dhidi ya mtoto wa kike alisema kati ya Januari na Desemba 2021 kulikuwa na makosa ya ubakaji 5899, ulawiti 152 na kutupa watoto 58 tofauti na mwaka 2022 uliokuwa na makosa 6335 ya ubakaji, 197 ya ulawiti na 70 ya kutupa watoto.

Na kwa upande wa mkoa wa Iringa, Nzuki alisema kati ya Januari na Desemba 2021 kulikuwa na matukio 175 ya ubakaji na moja la kutupa mtoto huku mwaka 2022 yakiripotiwa matukio matatu ya mauaji, 217 ya kubaka na matatu ya kutupa watoto.

“Tunayo kazi kubwa ya kushusha makosa haya hususani ya kubaka katika mkoa huu na mikoa yote nchini. Tumeleta maofisa 200 wa dawati kutoka nchi nzima waliosambazwa mkoa mzima wa Iringa kwa ajili ya kutoa elimu dhidi ya vitendo hivyo,” alisema.

Aidha alisema dawati hilo limeanzisha miongozo na taratibu mbalimbali za kutoa huduma na katika kuwajengea uwezo askari wake ili waweze kushughulikia vyema changamoto hizo; Jeshi la Polisi lina somo linalojitegemea la ‘Jinsia na Ulinzi wa Mtoto’ linalotolewa katika mafunzo yote wanayopewa askari.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Halima Dendego aliitaka jamii kuwalinda na kuwathamini watoto wa kike ili wafikie ndoto zao ikiwemo ya kuwa viongozi wakubwa nchini kama walivyo wao.

“Tuwape ulinzi watoto wetu, tuwahatamie kama kuku anavyohatamia vifaranga vyake. Miongoni mwa watoto hawa wa kike wapo akina Mama Samia Suluhu Hassan wa baadae, mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya, na viongozi wengine wengi wa kike,” alisema.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Gorgea
Gorgea
1 month ago

Google pay 390$ reliably my last paycheck was $55000 working 10 hours out of consistently on the web. (nd)My increasingly youthful kinfolk mate has been averaging 20k all through continuous months and he works around 24 hours reliably. I can’t trust how direct it was once I attempted it out. This is my essential concern…:) GOOD LUCK
For more info visit………
.
. http://www.Smartcash1.com

LindaCaudle
LindaCaudle
1 month ago

I’ve gained only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, mtg I was very troubled and thankfully
following website___________ http://Www.Careers12.com

Last edited 1 month ago by LindaCaudle
Back to top button
2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x